Arsenal matumaini tele itajifufua ikipepetana na Southampton nyumbani Jumapili

Arsenal matumaini tele itajifufua ikipepetana na Southampton nyumbani Jumapili

LONDON, Uingereza

Na MASHIRIKA

Baada ya kusuasua hapo awali, Arsenal wameonyesha dalili za kurejesha hadhi yao baada ya kupanda kutoka eneo hatari na kukaribia nne bora.

Vijana hao wa Mikel Arteta wako pointi nne tu nyuma ya West Ham United wanaoshikilia nafasi ya nne jedwalini. Lakini kwa jumla matokeo yao kufikia sasa sio ya kujivunia baada ya kushindwa mara tatu katika mechi zao nne za karibuni za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Walishindwa na Liverpool, Manchester United na Everton.Ligi itakaporejelewa Jumapili, Arsenal watakuwa nyumbani kukabiliana na Sothampton ambao pia wanatatizika baada ya kwenmda mechi nne bila ushindi.Chini ya kocha Rlph Hasenhuttle, Southampton wameandikisha ushindi mara mbili dhidi ya Watford na Aston Villa, kabla ya kushindwa na Norwich City na Liverpool.

Walitoka sare na Leicester City na Brighton.Mwaka huu Arsenal wameshinda mara tatu nyumbani ukiwemo ushindi mara mbili bila kufungwa bao, ingawa washambuliaji wao akiwemo Martin Odegaard wamekuwa wakishindwa kufunga mabao.

Dhidi ya Southampton, Arsenal imeshinda mara tatu na kutoka sare mara mbili katika mechi tano, lakini itakumbukwa Southampton iliwabandua katika michuano ya FA Cup msimu uliopita. Isisahaulike Southampton haijawahi kushinda Arsenal tangu 1987.

Ratiba ya mechi za Jumapili ni Manchester City na Wolves, Chelsea na Leeds United, Liverpool na Aston Villa, Arsenal na Southampton, Norwich City na Manchester United, Burnley na West Ham United

You can share this post!

Mama na binti wakana kukwepa kulipa ushuru wa Sh2.2Bilioni

Barca nje ya 16-bora taji la UEFA

T L