Michezo

Arsenal waanza kunyanyaswa na miamba Bayern mechi ya Uefa

April 9th, 2024 1 min read

UPDATE: Mechi ilimalizika kwa sare ya 2-2 baada ya Arsenal kusawazisha kupitia mshambuliaji Leandro Trossard dakika ya 76

Na FATUMA BARIKI

VIONGOZI wa Ligi ya Uingereza Arsenal wamemaliza kipindi cha kwanza katika mechi ya robo fainali ya Uefa dhidi ya miamba wa Ujerumani Bayern Munich wakiwa wamenyukwa 2-1.

Kikosi cha The Gunners ambacho kilianza mchezo vyema kwa kujipatia bao kupitia kwa nyota Bukayo Saka katika dakika ya 12 kilianza kuyumba wakati wanabeki walipokosa kusomana na kuelewana kabla ya wavamizi wa Bayern kuchangamka haraka na kufunga bao la kusawazisha kupitia kwa mchezaji wa zamani wa Arsenal Serge Gnabry.

Chombo cha ‘Ndovu’ Arsenal, kama mashabiki wanavyojiita kwa utani, kimeonekana kuzamishwa kabisa kufuatia bao la pili la Bayern lililojazwa kimiani na mtani wao wa jadi aliyetokea Tottenham, Harry Kane wakati alipofunga penalti kufuatia kuangushwa kwa mchezaji wa Bayern kwenye kisanduku.

Mechi inaingia kipindi cha pili….