Arsenal wajiondoa kwenye Florida Cup baada ya kikosi kuambukizwa corona

Arsenal wajiondoa kwenye Florida Cup baada ya kikosi kuambukizwa corona

Na MASHIRIKA

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

ARSENAL wamefutilia mbali ziara yao ya kuelekea Amerika kwa ajili ya kujifua kwa kampeni za msimu ujao wa 2021-22.

Hii ni baada ya “idadi ndogo” ya wanasoka na maafisa wao wa benchi ya kiufundi kuambukizwa virusi vya corona.Chini ya kocha Mikel Arteta, Arsenal walikuwa wameratibiwa kuvaana na Inter Milan, Everton na Millonarios kwenye kipute cha Florida Cup.

Arsenal hawakutoa idadi kamili ya visa vya maambukizi hao katika kikosi chao.Kivumbi cha kuwania taji la Florida Cup kimeratibiwa kuanza Jumapili ya Julai 25 uwanjani Camping World, Orlando. Waandalizi wa kipute hicho bado hawajafichua iwapo mpinzani badala wa kujaza pengo la Arsenal ambao wamejiondoa amepatikana.

 

  • Tags

You can share this post!

Celtic na Midtjylland nguvu sawa kwenye mchujo wa UEFA

Afisa Mkuu Mtendaji wa AC Milan, Ivan Gazidis, augua...