Na MASHIRIKA
KOCHA Mikel Arteta amesema kikosi chake cha Arsenal “kina kiu ya kuridhisha msimu huu” baada ya kuanza kampeni zao za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Crystal Palace mnamo Ijumaa usiku ugani Selhurst Park.
Arsenal walitumia mchuano huo kuendeleza ubabe uliowashuhudia wakishinda mechi zote sita za kujiandaa kwa msimu mpya wa 2022-23. Walijiweka kifua mbele katika dakika ya 20 kupitia kwa Gabriel Martinelli aliyekamilisha kwa kicha mpira ambao pia alipokezwa kwa kichwa na sajili mpya, Oleksandr Zinchenko.
Ilichukua Crystal Palace ya kocha Patrick Vieira kuanza kuwatamalaki Arsenal ambao walimtegemea zaidi kipa Aaron Ramsdale kupangua makombora mazito aliyoelekezewa na wanasoka wa Palace – Joachim Andersen, Odsonne Edouard, Jordan Ayew na Wilfried Zaha.
Arsenal walipata bao la pili katika dakika ya 85 baada ya beki Marc Guehi kujifunga alipozidiwa ujanja na Bukayo Saka.
TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO