Arsenal wakomoa West Ham United na kuingia nne-bora EPL

Arsenal wakomoa West Ham United na kuingia nne-bora EPL

Na MASHIRIKA

ARSENAL waliweka hai matumaini ya kushiriki soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) msimu ujao baada ya kupepeta West Ham United 2-0 mnamo Jumatano usiku ugani Emirates na kuingia ndani ya mduara wa nne-bora kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Gabriel Martinelli alifungulia Arsenal ukurasa wa mabao mwanzoni mwa kipindi cha pili kabla ya kiungo mvamizi Emile Smith Rowe kutoka benchi na kuhakikishia waajiri wake ushindi huo.

Nahodha mpya wa Arsenal, Alexandre Lacazette pia alishuhudia penalti yake ya kipindi cha pili ikipanguliwa na kipa wa zamani wa Arsenal, Lukasz Fabianski katika kipindi cha pili.

West Ham walikamilisha mechi na wachezaji 10 pekee uwanjani baada ya Vladimir Coufal kuonyeshwa kadi ya pili ya manjani kutokana na kosa la kumchezea Lacazette visivyo ndani ya kijisanduku.

Coufal alikuwa tayari ameonyeshwa kadi ya kwanza ya manjano katika kipindi cha kwanza baada ya kumkabili beki Kieran Tierney visivyo.

Arsenal wangalifunga mabao zaidi katika kipindi cha pili kupitia kwa Tierney Martinelli, Bukayo Saka na Gabriel Magalhaes.

Kocha Mikel Arteta alidumisha kikosi alichokitegemea katika ushindi wa 3-0 uliosajiliwa na Arsenal dhidi ya Southampton mnamo Disemba 11, 2021 ugani Emirates.

Licha ya kuanza kampeni za msimu huu kwa matao ya juu, West Ham wameshinda mechi moja pekee kutokana na sita zilizopita ligini na kwa sasa wanashikilia nafasi ya nne kwa alama 29, moja kuliko West Ham na mbili zaidi kuliko nambari sita Manchester United United. Tottenham Hotspur wanakamata nafasi ya saba kwa pointi 25.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO 

You can share this post!

Kinda Caleb Atuta ajisuka akilenga kufikia viwango vya CR7

Haaland awabeba Dortmund dhidi ya Furth ligini

T L