Michezo

Arsenal wana nafasi finyu Ballon d’Or 2024, Manchester United hawapo kabisa

Na GEOFFREY ANENE September 5th, 2024 2 min read

MATUMAINI ya mchezaji kutoka Arsenal kushinda tuzo ya soka ya kifahari ya Ballon d’Or 2024 yanaonekana finyu sana licha ya kuwa ni mojawapo ya klabu zenye idadi kubwa ya wachezaji katika orodha ya wawaniaji 30.

Wanabunduki wa Arsenal wanajivunia kuwa na viungo Martin Odegaard na Declan Rice, winga Bukayo Saka na beki William Saliba katika orodha hiyo itakayopigiwa kura na waandishi wa soka kutoka mataifa 100-bora kwenye viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) ili kuchagua mshindi.

Jarida la France Football limeendesha tuzo hiyo tangu lianzishe mwaka 1956. Hakuna mchezaji wa Arsenal amewahi kuibuka mshindi wa tuzo hiyo.

Mfaransa Thierry Henry ndiye alikaribia sana kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Arsenal kupata tuzo hiyo alipomaliza nambari mbili nyuma ya Pavel Nedved (Juventus/Czech) mwaka 2003 na kukamata nafasi ya tatu mwaka 2006 nyuma ya Waitaliano Fabio Cannavaro (Real Madrid) na Ginaluigi Buffon (Juventus), mtawalia.

Katika orodha ya 30-bora wanaowania Ballon d’Or mwaka 2024, Mbrazil Vinicius Junior na Muingereza Jude Bellingham (Real Madrid), na Mhispania Rodri na Erling Haaland (Manchester City) wako katika orodha ya wanaopigiwa upatu kuibuka na ushindi.

Hakuna mchezaji kutoka Manchester United wala Liverpool yuko katika orodha ya 30-bora.

Mshindi mpya atapatikana mwaka huu kwa sababu bingwa mara nane Lionel Messi aliachwa nje.

Orodha ya wawaniaji 30-bora (Ballon d’Or 2024)

Jude Bellingham (Real Madrid/Uingereza), Ruben Dias    (Manchester City/Ureno), Phil Foden (Manchester City/Uingereza), Federico Valverde (Real Madrid/Uruguay), Emiliano Martinez (Aston Villa/Argentina), Erling Haaland (Manchester City/Norway), Nico Williams (Bilbao/Uhispania).

Wengine ni Granit Xhaka (Bayer Leverkusen/Uswisi), Artem Dovbyk (Roma/Ukraine), Toni Kroos (Real Madrid/Ujerumani), Vinicius Junior (Real Madrid/Brazil), Dani Olmo (Barcelona/Uhispania), Florian Wirtz (Bayer Leverkusen/Ujerumani), Martin Odegaard (Arsenal/Norway), Mats Hummels (Borussia Dortmund/Ujerumani), Rodri (Manchester City/Uhispania), Harry Kane (Bayern Munich /Uingereza), Declan Rice (Arsenal/Uingereza), Vitinha (PSG/Ureno).

Pia wapo Cole Palmer (Chelsea/Uingereza), Dani Carvajal (Real Madrid/Uhispania), Lamine Yamal (Barcelona/Uhispania), Bukayo Saka       (Arsenal/Uingereza), Hakan Calhanoglu (Inter Milan/Uturuki), William Saliba (Arsenal/Ufaransa), Kylian Mbappe (Real Madrid/Ufaransa), Lautaro Martinez (Inter Milan/Argentina), Ademola Lookman (Atalanta/Nigeria), Antonio Rudiger (Real Madrid/Ujeruamni) na  Alejandro Grimaldo  (Bayer Leverkusen/Uhispania).