Arsenal washauriwa kumuuza Aubameyang, kutafuta mvamizi mpya Januari 2022 na kumpa Tierney unahodha

Arsenal washauriwa kumuuza Aubameyang, kutafuta mvamizi mpya Januari 2022 na kumpa Tierney unahodha

Na MASHIRIKA

KIUNGO wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Frimpong ameshauri klabu hiyo kumtia mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang mnadani baada ya fowadi huyo raia wa Gabon kupokonywa utepe wa unahodha kwa sababu ya utovu wa nidhamu.

Sogora huyo wa zamani wa Borussia Dortmund aliachwa nje ya kikosi kilichotegemewa na Arsenal katika ushindi wa 2-0 dhidi ya West Ham United ugani Emirates mnamo Disemba 15, 2021

Mustakabali wa Aubameyang ugani Emirates sasa unamulikwa na vikosi vingi barani Ulaya huku Barcelona na Chelsea wakiwa tayari kumtwaa.

Sasa Frimpong aliyechezea Arsenal mara 16 baada ya kukwezwa ngazi kutoka akademia, ametataka kocha Mikel Arteta kushikinikiza usimamizi kumuuza Aubameyang mnamo Januari 2022 na kumpa beki Kieran Tierney ukapteni wa kikosi. Alexander Lacazette ndiye aliyevalia utepe wa unahodha wa Arsenal dhidi ya West Ham.

“Aubameyang amekuwa na mazoea ya kuchelewa kuripoti kambini. Huo si mfano mzuri kwa chipukizi wanaotegemea kujifunza kutoka kwake,” akasema Frimpong aliyestaafu soka mnamo 2019 kutokana na majeraha ya mara kwa mara.

Arsenal wanatarajiwa kujishughulisha vilivyo katika soko la uhamisho wa wachezaji mnamo Januari 2022 kwa matarajio kwambwa watajinasia huduma za fowadi matata zaidi. Frimpong anaamini kwamba sajili bora zaidi kwa Arsenal katika safu hiyo ya mbele ni Dusan Vlahovic wa Fiorentina au Erling Braut Haaland wa Dortmund.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Kibera Ladies Soccer yatawazwa mabingwa wa Grandpa Super Cup

Wawaniaji wa ugavana Bungoma njia panda kuhusu chama cha...

T L