Michezo

Arsenal yatandika Brentford 2-1 na kukaa juu ya jedwali

March 9th, 2024 1 min read

NA MASHIRIKA

KLABU ya Arsenal imeipiga Brentford 2-1 ugani Emirates mnamo Jumamosi hivyo kuendeleza rekodi yake nzuri ya kugawa dozi kali kwa wapinzani.

Mechi hiyo ilianza saa mbili na nusu usiku saa za Afrika Mashariki.

Arsenal walijipa bao la kwanza kupitia kwa Declan Rice kunako dakika ya 19.

Hata hivyo kabla ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza, Yoane Wissa alisawazishia Brentford kunako dakika nne za ziada zilizoongezwa baada ya 45 za kwanza.

Baada ya mapumziko timu hizo ziliendelea kushambuliana lakini mwisho wa siku vijana wa kocha Mikel Arteta wakapata bao la ushindi ambalo lilijazwa kimiani na Kai Havertz katika dakika ya 86 ya mchezo.

Mchezo dhidi ya Brentford ulikuwa ni mechi ya raundi ya 28 ya EPL msimu huu kwa Arsenal ambao sasa wanaongoza jedwali kwa alama 64 mbele ya Liverpool (alama 63) na Manchester City wanaofunga tatu bora kwa alama 62.

The Reds wakiwa katika nafasi ya pili watacheza dhidi ya City kesho Jumapili.