AS Roma ya kocha Jose Mourinho yashinda mechi tatu mfululizo katika Serie A

AS Roma ya kocha Jose Mourinho yashinda mechi tatu mfululizo katika Serie A

Na MASHIRIKA

FOWADI Tammy Abraham, 24, alifunga bao la ushindi na kuwezesha AS Roma kucharaza Torino 1-0 katika mchuano wa Ligi Kuu ya Italia (Serie A).

Mchuano huo ulikuwa wa tatu mfululizo kwa Roma ya kocha Jose Mourinho kusajili katika mashindano ya Serie A.

Kikosi hicho kwa sasa kinashikilia nafasi ya tano kwenye msimamo wa jedwali la Serie A kwa alama 25, tatu nyuma ya Atalanta wanaofunga orodha ya nne-bora.

Bao la Abraham aliyeagana na Chelsea mwishoni mwa muhula wa 2020-21, lilikuwa lake la tisa katika mashindano yote ya muhula akivalia jezi za Roma.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

MWALIMU WA WIKI: Nicholas Kilonzo, mwalimu mahiri

Man-United na Chelsea zatoka sare uwanjani Stamford Bridge

T L