Habari Mseto

Asema alimchapa kwa kutumia mihadarati

August 18th, 2020 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

MVULANA mwenye umri wa miaka 23 alishtakiwa Alhamisi kwa kumchapa mama yake mzazi na kumwumiza.

Gerald Mukiri Njoroge alikanusha shtaka na kuomba mahakama “iamuru apelekwe kituo cha kumrekebisha tabia kwa vile amelewa na mihandarati.”

Akaungama Mukiri , “ Mimi natumia mihandarati sana. Zimenilemea n ahata zimenipelekea kumpiga na kumjeruhi mama yangu mzazi.”

Alighairi matendo yake mbele hakimu mwandamizi mahakama ya Kibera Bw Charles Mwaniki Kamau na kusema “ Nitakuwa mwananchi mwema nikiwacha mihandarati. Mimi natumia papaya.”

Mshtakiwa huyo alikabiliwa na shtaka la kumpiga na kumjeruhi Rose Muthoni Wanjiru mnamo Agosti 9,2020.

Hakimu alimwachilia kwa dhamana ya Sh20,000 pesa tasilimu.

Atarudi kortini Agosti 31 2020 kupewa maelekezo zaidi.