Kimataifa

Ashangaza kumbaka mamake kusherehekea kuachiliwa kutoka jela

July 24th, 2019 1 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU

MWANAMUME kutoka Ukraine alimbaka mamake mzazi, kusherehekea baada ya kuachiliwa kutoka jela, alikokuwa amefungwa kwa makosa ya mauaji.

Vitaliy, 42, alimvamia mamake alipokuwa amelala na kumtendea unyama huo.

Hii ilikuwa baada ya kutoka jela. Alikuwa amefungwa kwa kupatikana na hatia ya kumchapa mwanamume hadi kufa, lakini akaachiliwa huru mnamo Mei.

Mamake mshukiwa ambaye ana miaka 62 alifurahia kurejea nyumbani kwa mwanawe hadi akaandaa karamu, lakini baadaye usiku huo mshukiwa anasemekana kumvamia na kumbaka.

Alikamatwa alipokuwa amejificha, na sasa anahatarisha kufungwa miaka mitano akipatikana na hatia hiyo.

Mamake alimkana na kusema kuwa hatamchukua kama mwanawe tena.

“Baadhi ya marafiki zake walikuja katika karamu, tulipata vinywaji na tukafurahia, kila kitu kilikuwa shwari. Lakini usiku baada ya wageni kuondoka alinivamia,” akasema mama huyo.

Alisema baada ya kuwaaga wageni alirejea chumba chake cha kulala, lakini saa chache mwanawe akamvamia. Alisema juhudi zake za kukataa ziligonga mwamba, kwani mshukiwa alimchapa.

Msemaji wa polisi Yury Sulaev alisema kuwa mshukiwa alishtakiwa kwa ubakaji na akazuiliwa.

“Ako hatarini kufungwa miaka mitano akipatikana na hatia. Uchunguzi unaendelea,” akasema Sulaev.