Dondoo

Ashangaza kumpa mke idhini kugawia makalameni asali

November 22nd, 2018 1 min read

NA BENSON MATHEKA

Kirigiti, Kiambu

BUDA wa hapa aliwashangaza wakazi walipobaini kwamba alimwambia mkewe atafute mpango wa kando wa kumlisha uroda.

Inasemekana jamaa alifikia uamuzi huo kufuatia lalama za mkewe kwamba alikuwa amemkausha kwa muda mrefu bila ya kumtimizia tendo la ndoa.

Kulingana na mdokezi, jamaa alikuwa akikidhi mahitaji yote ya nyumbani lakini ilibainika kuwa alikuwa mzembe wa shughuli za chumbani.

“Kusema ukweli, jamaa ana bidii ya kutafuta mali, mkewe huvaa mavazi ya pesa nyingi, ana gari alilonunuliwa na mumewe na kila wakati hupatiwa pesa za kutosha.”

“Hata hivyo, hakuna aliyekuwa akibaini kwamba mwanadada huyo alikuwa akisononeka kwa kukosa kurusha roho hadi juzi alipomlalamikia mumewe kwa kumpuuza kwa siku nyingi,” alisema mdokezi.

Penyenye zinaarifu kwamba mwanadada alipodai haki yake ya kutoka kimapenzi na mumewe, jamaa alimwambia hakuwa na wakati wa kula uroda.

“Mwanadada alishangaza mama mkwe alipomfahamisha kuwa mumewe alimweleza kwamba hakuwa na wakati wa kushiriki tendo la ndoa. Alimwambia hufika nyumbani akiwa amechoka kwa sababu akili yake hufikiria biashara tu na kumtaka atafute mwanamume wa kuzima ashiki zake ikiwa hawezi kuvumilia,” mdokezi alieleza.

Inasemekana kuwa mama mkwe aliamua kumweleza mumewe na wakamuita mwanao kumshauri lakini jamaa alisisitiza kuwa hakuwa na wakati wa kuharibu akirushana roho.

“Nitashughulika na biashara zangu zinazonipatia pesa za kumtunza mwanamke huyo kuwa jinsi alivyo au nitaziacha ili kufanya mapenzi. Ikiwa hapendezwi na bidii yangu ya kutafuta pesa, ana haki ya kutafuta mwanamume mwingine wa kumpa raha anayotaka ikiwa kwake raha ni kulishwa uroda pekee,” mdokezi alisema akinukuu jamaa alivyowaeleza wazazi wake.

Inasemekana wazazi walisema hawatachoka kumshauri mwana wao kumtimizia mkewe haki ya ndoa.