Habari Mseto

Ashangaza kumuua mkewe kisha kujiua

October 12th, 2020 1 min read

NA STANELY NGOTHO

Wingu la majonzi lilitanda eneo la Kimarat, Kitengela baada ya mwanaume kumuua mkewe kabla ya kujitia kitanzi.

Timothy Weru, wa miaka 35 alisemekana kumuua mkewe wa miaka 23 Miriam Nyakaro baada ya kurudi nyumbani kwao baada ya wiki kadhaa za kutengana.

Jamaa zake walisema kwamba wawli hao wamekuwa na matatizo ya ndoa yaliyopeleka mama huyo wa watoto wawili kutoroka nyumbani kwao mara kadhaa.

Kulingana na majirani mwanamke huyo aliyekuwa akifanya kazi kwenye duka la M-Pesa alipofika nyumbani kwake hapo ndipo matatizo yalianza.

Mwanamune huyo alishika na kumpiga kichwani kwa kutumia nyundo. Mwanume huyo alimdunga mara kadhaa huku majirani wakiangalia  hadi kifo.

Majirani walisema kwamba mwanaume huyo alitishia kuwaua wakijaribu kuingililia kumwokoa Nyakaro.

Ili kuhepa mkutano wa watu uliokuwa umeanza kuwa mkubwa alikimbia kwenye uwanja uliokuwa karibu na kujidunga kisu kifuani na kufariki.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA