Habari Mseto

Ashtakiwa kuiba mafuta ya injini

August 18th, 2020 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

MFANYAKAZI katika duka la kuuza bidhaa za mafuta ya petroli alifikishwa kortini kwa wizi wa katoni 13 za mafuta ya injini aina ya Shell Rimula R2 yenye thamani ya Sh51,385.

David Kariuki aliyefikishwa kortini akiwa amevaa gauni nyekundu ya kazini alikana shtaka hilo mbele ya hakimu mwandamizi Charles Mwaniki Kamau katika mahakama ya Kibera Nairobi.

Kiongozi wa mashtaka Bw Geoffrey Obiri alimweleza hakimu , makatoni hayo ya mafuta ya magari yamefikishwa mahakamani kutolewa kama ushahidi ndipo yarudishiwe mwenyewe Bw Nites Valyi Pindoria akayauze.

Pia Bw Obiri alieleza mahakama hapingi mshtakiwa akiachiliwa kwa dhamana.

Bw Mwaniki alimwachilia mshtakiwa kwa dhamana ya Sh50,000.

Mahakama iliamuru ushahidi aliokamatwa nao mshtakiwa uwekwe katika stoo ya korti ndipo ukitolewa kortini mlalamishi arudishiwe.

Siku ya kusikizwa kwa kesi hiyo itatengwa Agosti 31,2020.