Habari Mseto

Ashtakiwa kukuza bangi nyumbani

August 20th, 2020 1 min read

Na Richard Munguti

Mvulana mwenye umri wa miaka 25 alifikishwa kortini kwa kukuza bangi shambani mwake.

James Orengo Nzau alikabiliwa na shtaka la kukuza mmea wa Bhangi katika kijiju cha Ngandu eneo la Dagoreti kaunti ya Nairobi.

Nzau alikana kuendeleza kilimo cha bhangi Nairobi.

“Bangi hii iliyo mbele ya mahakama ya gunia moja sio yangu..ni ya jirani yangu. Mimj sikuzi bhangi na wala siivuti.”

Mshtakiwa aliomba aachiliwe kwa dhamana.

Kiongozi wa mashtaka aliomba korti iamuru bhangi ipelekwe kwa wataalam katika maabara ta Serikali ikapimwe kuthibitisha ni bhangi.

Hakimu mkuu aliamuru bhangi ipelekwe kwa maabara ya Serikali kupimwa na ripoti kufikishwa kortini baada ya wiki mbili.

Mshtakiwa aliachiliwa kwa dhamana ya Sh100000.