Habari Mseto

Ashtakiwa kumdunga mumewe kisu tumboni

August 21st, 2020 1 min read

Na Richard Munguti

Mwanamke mwenye umri wa miaka 22 alikana shtaka la kumdunga mumewe kisu tumboni matumbo yakatoke.

Ebby Khalea alifikishwa mbele ya hakimu mkuu Abdulkadir Lorot Ijumaa. Shtaka dhidi yake ni kuwa alimwumiza mumewe Michael Ngure Wanjeri na kumpa jeraha la kudumu..

“Je, mlalamishi aliumia aje?” Lorot aliuliza.

“Kulingana ripoti ya matibabu kutoka hospitali ya Mama Lucy mlalamishi alidungwa kisu tumboni..Kwa sasa hawezi kutembea barabara,” alisema kiongozi wa mashtaka Geoffrey Obiri.

Bw Obiri aliongeza kusema mlalamishi alipata jeraha la kudunu

“Mlalamishi angali anaendelea kupitia matibabu katika hospitali,” alisema Bw Obiri.

Akitoa uamuzi hakimu alisema mshtakiwa ataachiliwa kwa dhamana ya Sh100000, kesi itatajwa tena Septemba 4