Habari Mseto

Ashtakiwa kumjeruhi aliyenyakua mumewe

August 26th, 2020 1 min read

NA Joseph Ndunda

Mwanamke wa miaka 20 ameshtakikwa kwa kumsababishia  majerahamwanamke mwezake  kwa kumdunga kisu akimlaumu  kwa kumchukua mpeziwe.

Catherine Njeri Wanjiru alistakiwa kwa kumuumiza Sharon Iminza Malela nje ya nyumba ya mpeziwe Alvin Jumba Mitsami  Zimmerman Kasarani Nairobi Januari 4.

Alishtakiwa pamoja na Bw Mitsami. Bi Wanjiru alisema kwamba mwathiriwa alikuwa amekuja na wanaume watatu kuwavamia kwasababu ya kuishi na Mitsami wakiwa bado wachumba.

Mitsami alikuwa amempigia Malela simu aende nyumbani kwake hapo ndipo alipata Wanjiru akiwa amemgoja akiwa na kisu mkononi.Vita ilizuka huku Mitsami huku akimzuia Wanjiru kumdunga kisu Malela.

Baadaye Wanjiru alimfuata Malela na kumdunga kisu mgogoni ambapo alipata majeraha mabaya.Mwathiriwa alikimbiwa hospitali ambapo alilazwa.

Wawili hao Wanjiru na Mitsami walikana mashtaka hayo mbele ya jaji Derrick Kuto korti ya Kibera.

Waliachiliwa kwa dhamana ya Sh 400,000 kila mmoja huku kesi ikitajwa tena Septemba 17.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA