Habari Mseto

Ashtakiwa kumlaghai mwenzake hela za kununua mitumba

August 21st, 2020 1 min read

Na Richard Munguti

Tarishi wa kubeba vifurushi vya nguo kuu kuu almaarufu mitumba katika la Gikomba alishtakiwa kumlaghai John Muhora Maina Sh353,000 akidai atamnunulia robota tatu za mitumba.

“Mheshimiwa sikuiba pesa hizo.Mfuko wa suruali yangu ulipasuliwa kwa wembe nikiwa nimebeba kifurushu cha mitumba.Sikuiba kamwe,” Junior alimweleza hakimu mkuu Abdulkadir Lorot.

Mshtakiwa aliomba aachiliwe kwa dhamana Ijumaa aliposhtakiwa katika mahakama ya Kibera.

Hakimu allimwachilia kwa dhamana ya Sh300,000.

Kesi itatajwa Septemba 4.