Habari Mseto

Ashtakiwa kumumunya maelfu ya watu mitandaoni

April 17th, 2020 1 min read

NA RICHARD MUNGUTI

Muuzaji bidhaa kupitia mutandao ya kijamii Antony Njenga Wanjiku alishtakiwa kuwapunja wateja wanne zaidi ya Sh132,000.

Alikanusha shtaka la kumlaghai Isaac Okumu Sh55000 akidai atamuuzia televisheni ya inchi 65.

Shtaka lilisema nshtakiwa alilipwa kwa njia ya Mpesa. Hakumpelekea Okumu runinga hiyo kama alvyomuahidi..

Shtaka la pili lilikuwa mshtakiwa alimkomoa Benson Kilonzo Sh13,000 akidai atampelekea runinga katika makazi yake na jiko la kupikia na gesi

Shtaka la tatu mi kwamba alimlaghai Leah Muthoni Mutahi Sh34,000 akidai atamuuzia televisheni muundo wa Hisence ya inchi 55.

Hakuipeleka kama alivyomuahidi Muthoni.

Shtaka la nne lilisema alimlaghai Rita Wanja sh30,000 akidai atamuuzia mtungi wa gesi.

Mshtakiwa aliomba aachiliwe kwa dhamana akisema “nimeoa na mke wangu na watoto wananitegemea.”

Kiongozi wa mashtaka hakupinga ombi la mshtakiwa kuachiliwa kwa dhamana.

Hakimu alimwachilia kwa dhamana ya Sh100, 000. Kesi itatajwa Aprili 30.