Ashtakiwa kutumia kitambulisho cha wizi kujisajili katika mtandao wa Mpesa

Ashtakiwa kutumia kitambulisho cha wizi kujisajili katika mtandao wa Mpesa

Na RICHARD MUNGUTI

MCHUNGAJI wa mifugo alishtakiwa Jumanne kwa kutumia kitambulisho cha mtu mwingine kujisajili katika mtandao wa Mpesa.

Bw Ambrose Kibewa Bunyinge almaarufu Juda Kathunkumi Kithinji alishtakiwa mbele ya hakimu mwandamizi David Ndungi.Bunyinge aliyekiri shtaka punde tu alibadilisha nia baada ya kusikia kiongozi wa mashtaka akiomba mahakama imsukume jela.

Bunyinge alikabiliwa na shtaka la kutumia kinyume cha sheria kujisajili katika kampuni ya Safaricom kuwa akipokea pesa katika mtandao wa Mpesa.Alipoulizwa na hakimu iwapo alifanya hivyo mshtakiwa alisema ,”niliokota vitambulisho vitatu kisha nikatumia kile cha Juda.”

Alieleza mahakama kwamba alikuwa ameajiriwa na Juda kulisha mifugo katika kaunti ya Nakuru.“Nilipoajiriwa nilikuwa na umri mdogo. Singelipewa kitambulisho. Nilichukua kitambulisho cha Juda kukitumia kujisajili katika mtandao wa Mpesa.

Sikuwa na nia ya kukitumia kwa njia nyingine,” alisema Bunyinge.Punde aliposema kuwa aliokota vitambulisho kadhaa na hakutarajia kukitumia kwa wizi Bw Ndungi alimweleza amekana shtaka kisha akapewa dhamana ya Sh300,000 afanye kesi akiwa nje.

Mshtakiwa alikana alijaribu kujiandikisha katika mtandao wa Mpesa katika mji wa Kehancha kaunti ya Migori siku isiyojulikana.Hata hivyo alikamatwa akiwa jijini Nairobi akiwa na kitambulisho kisicho chake.

Kesi itatajwa baada ya wiki mbili itengewe siku ya kusikizwa.

  • Tags

You can share this post!

Washtakiwa wenza wa Mbunge Rigathi Gachagua wakana ufisadi...

Wataalam wa maabara kizimbani kwa vyeti feki