Asimulia alivyofunza kutumia sanaa kurembesha vifaa

Asimulia alivyofunza kutumia sanaa kurembesha vifaa

Na MAGDALENE WANJA

Alipokuwa akikua, Bi Naomi Namayi alikuwa na ndoto ya kufanya kazi katika idara ya upelelezi kama afisa wa uchunguzi.

Ili kuafikia ndoto hii, alisoma na hata kupata shahada ya Criminology and Security Studies katika chuo kikuu.

Baada ya kukamilisha masomoyake, alifanya kazi katika mahakama ya Nakuru, ila aliacha baada ya muda mfupi kutokana na kile alitaja kama kutoridhika.

Baadaye alijiunga na shirika la kibinafsi jijini Nairobi ila kazi hio pia alijiuzulu baada ya muda mfupi.

“Niligundua kwamba kazi hii haikuwa inaridhisha kama vile nilivyoiona katika filamu. Humu nchini, kazi hio ni tofauti sana na imejaa changamoto tele,” alisema Bi Namayi.

Bi Namayi alizaliwa mjini Nakuru ila alipata nafasi ya kusafiri na kuzuru nchi mbalimbali ambako aliweza kujifunza mambo mengi kama vile aina mbalimbali za sanaa.

Baaa ya kujiuzulu, aliamua kujaribu mojawapo ya sanaa ijulikanayo kama Resin Art, inayotumia mseto wa chembechembe kutoka kwa miti na kemikali.

“Niligundua aina hii ya sanaa mnamo mwaka 2019 nilipokuwa nikitafuta aina mbalimbali za sanaa ambayo ningetumia kuifanya nyumba yangu kuvutia,” alisema Bi Namayi.

Hakupokea mafunzo yoyote ila aliaza kujifunza mwenyewe jinsi ya kutengeneza mapambo ya nyumbani. Baada ya kutengeneza mapambo kadhaa, aliweza kupata wateja ambao walivutiwa na kazi yake.

Hii iimfanya kutia bidii Zaidi na kujifunza miundo ya aina tofauti huku akiongeza modoidi zaidi. Aina hii ya sanaa huhitaji chembechembe kadhaa vya kuboresha kazi yake.  Vifaa vingine anavyotumiani pamoja na mbao, turubai na silicon.

“Kazi hii huchukua muda wa masaa 24 kukauka ili kupata umbo linalofaa na ambalo haliwezi kuharibika kwa kuguswa,” aliongeza Bi Namayi.

 Wateja wake sana sana huwa ni watu amabao wanapenda kazi ya sanaa.

Ata hivyo kazi hii inachangamoto kama vile ukosefu wa vifaa vya kutumia amabavyo kulingana na Bi Namayi, huwa ni ghali na wakati mwingine havipatikani kabisa humu nchini.

 Bi Namayi hutumia kurasa zake za mtandao kuwauzia wateja kazi yake ambapo pia hupata maagizo kutoka kwa wateja ambao wanatamani kazi ile.

Kila muundo huuzwa kwa bei tofauti ambayo hutegemea aina ya nyezo zilizotumika na muda aliouchukua kukamilisha.

You can share this post!

Timu tatu za voliboli kukosa mastaa kwenye kipute muhimu

Mawakili wamtoroka Sonko tena