Habari Mseto

Askari wa Utawala amuua mkewe kabla kujiua kwa risasi

November 7th, 2018 1 min read

Na JOSEPH OPENDA

AFISA wa polisi wa utawala katika kambi ya Piave, Kaunti ya Nakuru, alimuua mkewe kwa kumpiga risasi kisha akajiua kwa risasi katika hali isiyoeleweka.

Ilisemekana wawili hao walikuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa miezi mitatu iliyopita na tayari wameoana.

Kulingana na wakazi wa eneo hilo, milio miwili ya risasi ilisikika Jumatatu jioni lakini hakuna aliyejali kuchunguza kilichofanyika wakati huo. Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Nakuru, Bw Hassan Barua, alisema miili hiyo miwili ilipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Nakuru jana kusubiri kufanyiwa upasuaji huku uchunguzi ukianzishwa.