Askofu akubali atamlea na kumtunza mtoto aliyezaa na mshiriki na akaitkia

Askofu akubali atamlea na kumtunza mtoto aliyezaa na mshiriki na akaitkia

Na RICHARD MUNGUTI

ASKOFU aliyeshtakiwa na mshiriki kwa kumpachika mimba amekubali kumlea mtoto huyo na kukimu mahitaji yake yote.

Askofu David Muriithi Munyaka ameeleza katika ushahidi aliowasilisha kortini alishtuka alipoelezwa na mlalamishi kwamba amejifungua  ilhali alikuwa akidai yuko na ufimbe tumboni kwa lugha ya kimatibabu-Fibrod-Katika afivaditi aliyowasilisha mahakama ya Milimani , Askofu Mureithi, alidokeza kujifungua kwa mlalamishi huyo kumebaini alikuwa anadanganya hawezi kuzaa.

Muhubiri huyo amekiri alikuwa na uhusiano na mlalamishi kwa kipindi kifupi kisha wakaachana.“Nilipomfahamu mlalamishi alikuwa akiishi pamoja na mtoto mwingine aliyekuwa amemzaa,”asema Askofu huyo wa kanisa moja la kipendekoste jijini.

Kinyume na dhana potovu ya mlalamishi kwamba yeye (askofu) ni tajiri anayeishi maisha ya kifahari, muhubiri huyu amefichua hana mapato makubwa kwa vile “ halipwi mshahara na hutengemea tu zawadi zinazoletwa na washirika kanisani.”

Askofu ameungama kwamba ameoa na yuko mke na watoto.Hata hivyo amesema kama mtu mwenye busara atamlea mtoto huyo na kughramia mahitaji yake.“Siwezi pata Sh100,000 anazodai mlalamishi niwe nikimlipa kila mwezi,” alisema Askofu Muriithi.

Alikiri kuwa yeye ni Mtumishi wa Mungu anayewategemea washiriki kukimu mahitaji, amesema kamwe hawezi pata pesa za kuwekea mtoto huyo mwenye umri wa miaka miwili DSTV na kuwaweka katika maisha ya hali ya juu ambayo mlalamishi amepotoshwa na wanaomshauri.

Askofu huyo alishtakiwa na wakili Danstan Omari akiomba Askofu huyo ashurutishwe na mahakama kugharamia elimu na mahitaji mengine yote ya mtoto huyo.Pasta huyo amesema kabla ya kuanza uhusiano na mlalamishi, alimpata akijilipia nyumba na kugharamia mahitaji ya kifungua mimba wake.

“Naomba mahakama isitipotoshwe na dhamana mimi ni tajiri wa kupindikua na mlalamishi anataka apate mgawo wa mali zangu,” asema mshtakiwa.

  • Tags

You can share this post!

Yordenis Ugas wa Cuba amnyuka Many Pacquiao wa Ufilipino na...

WANGARI: Mabadiliko katika NHIF yawe ya kumfaidi mwananchi