Aston Villa watoka nyuma na kulazimishia Man-Utd sare ya 2-2 ligini

Aston Villa watoka nyuma na kulazimishia Man-Utd sare ya 2-2 ligini

Na MASHIRIKA

PHILIPPE Coutinho alifunga bao la dakika za mwisho na kusawazishia Aston Villa dhidi ya Manchester United katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) iliyoshuhudia masogora wa kocha Steven Gerrard wakitoka nyuma kwa mabao 2-0.

Coutinho alikuwa akijiandaa kuingia uwanjani kiungo mvamizi Bruno Fernandes alipofungia Man-United bao la pili katika dakika ya 67. Sogora huyo raia wa Ureno aliwaweka Man-United kifua mbele katika dakika ya sita kupitia mpira wa ikabu uliombabatiza kipa Emiliano Martinez na kujaa wavuni.

Ujio wa Coutinho aliyesajiliwa kwa mkopo kutoka Barcelona, ulifufua makali ya Villa waliorejeshwa mchezoni na Jacob Ramsey katika dakika ya 77.

Kutokuwepo kwa Cristiano Ronaldo kulimweka kocha mshikilizi Ralf Rangnick katika ulazima wa kutegemea maarifa ya chipukizi raia wa Uswidi, Anthony Elanga, 19, katika safu ya mbele akishirikiana na Edinson Cavani.

Man-United ambao sasa wamejizolea alama tano pekee kutokana na mechi nne zilizopita za EPL wanakamata nafasi ya saba jedwalini kwa pointi 32, moja nyuma ya Tottenham Hotspur. Arsenal wanashikilia nafasi ya tano kwa alama 35, mbili nyuma ya West Ham United wanaofunga orodha ya nne-bora. Villa kwa upande wao wanakamata nafasi ya 13 kwa alama 23 sawa na limbukeni Brentford.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Okutoyi aduwazwa na mnyonge Australia, asema ni funzo

AFCON: Nigeria yanyoa Sudan katika Kundi D na kuingia...

T L