Atalanta yapiga Juventus nyumbani kwa mara ya kwanza tangu 1989

Atalanta yapiga Juventus nyumbani kwa mara ya kwanza tangu 1989

Na MASHIRIKA

JUVENTUS walishuka hadi nafasi ya nane kwa alama 21 baada ya kupoteza mchuano wao wa tano kati ya 14 za Ligi Kuu ya Italia (Serie A) msimu huu walipopigwa 1-0 na Atalanta mnamo Jumamosi jijini Turin.

Ushindi wa Atalanta uliendeleza rekodi ya kutopigwa kwao katika mechi nane mfululizo na sasa wanakamata nafasi ya nne kwa pointi 28, tatu nyuma ya mabingwa watetezi Inter Milan wanaofunga mduara wa tatu-bora.  Bao la pekee na la ushindi lilifumwa wavuni na Duvan Zapata katika dakika ya 28. Ilikuwa mara ya kwanza tangu 1989 kwa Atalanta kupiga Juventus nyumbani.

Chini ya kocha Massimiliano Allegri, Juventus kwa sasa wamefunga mabao 18 pekee kutokana na mechi 14 za Serie A. Hiyo ndiyo idadi ndogo zaidi ya magoli yanayojivuniwa na vikosi vinavyoshikilia nafasi 10 za kwanza kwenye jedwali la Serie A.

Chombo cha Juventus kilizamishwa na Atlanta siku tatu baada ya Chelsea kuwakomoa 4-0 katika Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

You can share this post!

Depay na Coutinho wabeba Barcelona dhidi ya Villarreal...

Haaland aweka rekodi ya kuwa mwanasoka mchanga zaidi...

T L