Kimataifa

Ataliki mkewe baada ya kumfumania na mpango wa kando kwenye Google Street View

November 14th, 2018 1 min read

MASHIRIKA na PETER MBURU

MWANAMUME mmoja kutoka Peru alipigwa na butwaa ya maisha wakati alimpata mkewe akijiburudisha na mwanaume mwingine barabarani, wakati alipokuwa akitumia mtandao kupata ramani ya kwenda mahali Fulani.

Mwanaume huyo alikuwa akitumia mtandao wa Google Street View kutafuta njia rahisi ya kwenda daraja moja eneo la Lima, ndipo akaona picha ya mkewe akiwa ameketi kwenye kiti cha kupumzika huku akipapasa nywele za mwanaume ambaye alikuwa amelala na kuwekelea kichwa mapajani pa mwanamke huyo.

Picha hiyo inasemekana kuwa ilipigwa 2013.

Baada ya kumkabili, mkewe alikiri kuwa alikuwa na uhusiano siku za mbeleni.

Habari za mashirika ya nchi hiyo zilisema kuwa mwanaume huyo baadaye alimpa talaka mkewe huyo. Baadaye alichapisha picha hizo kwenye mitandao ya kijamii, picha zilizovutia matamshi makali dhidi ya mwanamke huyo kutoka kwa watumizi.

Mtandao wa Google Street View ambao huwasaidia watu wengi kupata ramani mara kadha umejipata kunakili visa vya kushangaza na vituko ambavyo kamera zake zilishika zilipokuwa zikirekodi.

Google Street View hutumia kamera za hali ya juu zikiwa kwenye magari na sehemu nyingine kwa digii 360 ili kupata pande zote za picha Fulani, kasha picha hizo zinaweza kumsaidia mtu kupata ramani kwa kutumia kompyuta ama simu zilizo na uwezo wa kufika intaneti.