Habari Mseto

Atoroka kutoka kituo cha karantini, wawili wafariki

August 24th, 2020 1 min read

NA BRIAN OJAMAA

Mtu mmoja aliyekamatwa kwa kukuiuka masharti ya kafyu yaliyowekwa ili kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona na kuwekwa kwenye vituo vya kutenga watu wa corona kwenye chuo cha kufunza madaktari cha Webuye, Kaunti ya Bungoma ametoroka.

Afisa wa maswala ya afya na usafi kaunti hiyo alisema kwamba mtu huyo alikamatwa na maafisa wa usalama wa kituo cha polisi na kupelekwa kwenye kituo cha afya.

“Alihepa kupitia dirisha la choo. Nalaumu maafisa wa usalama kwa tukio hilo,” alisema Dkt Walela.

Alizungumza akiwa kwenye mazishi eneo bunge ya Bumula Tulumba Ijumaa kwenye mazishi ya Chifu Sudi Namachanja .

Dr Walela alisema kwamba mtu mmoja aliyelazwa kwenye kituo hicho alifariki.

“Mtu huyo wa miaka 53 kutoka Kijiji cha Lugulu alikuwa kwenye matibabu kwenye hospitali ya Webuye lakini kwa magonjwa mengine alipelekwa kwenye kituo cha karantini lakini alianguka na kufariki baadaye,”alisema.

Alisema pia mtu mwingine alianguka na kufariki karibu na chuo kikuu cha Masinde Murilo Webuye baada ya kupatikana na matatizo ya kupumua.

“Kwa sasa tumechukua sampuli za mwendazake na kuzipeleka kwenye kituo cha uchunguzi cha Kemri kuchunguza kama alifariki kwa virusi vya corona,” afisa huyo alisema.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA