Boda atupwa nje kwa kutafuna muguka huku ibada ikiendelea

Boda atupwa nje kwa kutafuna muguka huku ibada ikiendelea

Na CHARLES ONGADI

MAJAONI, MOMBASA

BODABODA mmoja wa hapa alifurushwa kutoka kanisani kwa kutafuna muguka mahubiri yakiendelea.

Jamaa huyo alionekana akiingia kanisani bila wasiwasi akiwa na kifurushi mkononi na akajibanza katika viti vya nyuma pasta akichapa injili.

Dakika chache baada ya kuingia kanisani, alionekana akifungua kifurushi chake na kuchomoa veve akaanza kutafuna kana kwamba alikuwa katika baa.

Baadhi ya waumini waliamua ni heri lawama kuliko fedheha.

“Aisee, hapa siyo maskani ya kutafunia muguka bali nyumba ya Mungu inayostahili heshima,” muumini mmoja alisikika akisema kwa hasira.

Bila hili wala lile, jamaa alibebwa juu kwa juu na kutupwa nje ya kanisa.Hata hivyo, baada ya kurudiwa na fahamu zake bodaboda huyo alisema alikuwa akitafuna veve kufukuza usingizi baada ya kufanya kazi usiku.

“Nilifika hapa kanisani kupokea miujiza yangu baada ya kufanya kazi usiku na mchana na nikatumia muguka ili nisisinzie injili ikiendelea.” jamaa alidai.

You can share this post!

Kiunjuri awaonya Ruto na Raila kuhusu wawaniaji

TAHARIRI: Aibu wanasiasa kumwaga pesa njaa ikikeketa

F M