Michezo

Auba alenga kumaliza msimu kwa mabao mengi zaidi

April 16th, 2019 1 min read

NA CECIL ODONGO

MSHAMBULIZI wa Arsenal Pierre- Emerick Aubameyang amesema analenga kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) na kuwapiku Sergio Aguero na Mohamed Salah ambao wanaongoza chati ya wafungaji wa ligi hadi sasa.

Aubameyang alitumia kosa la mnyakaji wa Watford Ben Foster katika dakika ya 10 na kufunga bao uwanjani Vicarage Road Jumatatu Aprili 15 na kupatia Arsenal ushindi uliowapaisha hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa jedwali la EPL.

Watford walipata pigo kubwa katika mechi hiyo baada ya mshambulizi wao tegemeo Troy Deeney kulishwa kadi nyekundu dakika tatu baada ya Arsenal kupata goli.

Hata hivyo juhudi za mshambulizi Javi Gracia kuwafungia mabao zaidi ziligonga mwamba pale shuti lake lilipogonga mlingoti mara mbili huku mashambulizi mengine yakikosa kuzaa matunda.

“Nina imani ya kuwapiki Salah na Aguero kwenye mbio za kufukuzia mfungaji bora wa ligi. Najua kila mtu anajitahidi kutwaa kiatu cha dhahabu lakini nitaendelea kutia bidii hadi nitimize matarajio yangu. Nimefurahi sana kufunga bao hili kutokana na masihara ya kipa wao, lilikuwa bao zuri,” akasema Aubameyang.

Iwapo ataibuka mfungaji bora msimu huu wa 2018/19, mshambulizi huyo wa zamani wa Borussia Dortmund atarejesha kumbukumbu ya msimu wa 2017-17 kwenye ligi ya Ujerumani(Bundesliga) alipotwaa kiatu cha dhahabu kwa kutia wavuni mabao 31.

Hata hivyo alikiri kwamba kupangwa kwake na mshambulizi mwenzake Alexandre Lacazette kutaimarisha uwezo wake wa kuyafunga mabao mengi na kuwapiku wapinzani wake