Augsburg yaduwaza Bayern Munich ligini

Augsburg yaduwaza Bayern Munich ligini

Na MASHIRIKA

BAYERN Munich waliduwazwa na Augsburg kwa kichapo cha 1-0 katika Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) mnamo Jumamosi.

Kichapo hicho ambacho kilikuwa cha kwanza kwa Bayern msimu huu, kiliwanyima fursa ya kupaa hadi kileleni mwa jedwali la Bundesliga.

Mergim Berisha alifungia Augsburg bao la pekee na la ushindi katika pambano hilo lililokuwa lao la kwanza kushinda katika uwanja wa nyumbani muhula huu.

Bayern kwa sasa wamekosa kushinda mechi yoyote kati ya nne zilizopita ligini na huenda ikajikuta nje ya mduara wa nne-bora baada ya mechi za Jumapili kutandazwa.

Borussia Dortmund wanaselelea kileleni mwa jedwali la Bundesliga kwa alama 15 baada ya kucharaza Schalke 1-0. Youssoufa Moukoko, 17, alitokea benchi na kufunga bao la Dortmund. Mchezaji huyo ndiye mchanga zaidi kuwahi kufunga bao katika mechi kati ya Dortmund na watani wao Schalke.

Union Berlin ambao kwa sasa wanakamata nafasi ya pili kwa alama 14, huenda wakarejea kileleni mwa jedwali la Bundesliga iwapo watakomoa Wolfsburg mnamo Septemba 18, 2022. SC Freiburg wanaoshikilia nafasi ya tatu kwa pointi 13, moja zaidi kuliko Bayern, watachuana na Hoffenheim ugenini.

MATOKEO YA BUNDESLIGA (Jumamosi):

Augsburg 1-0 Bayern

Leverkusen 1-1 Werder Bremen

Borussia Dortmund 1-0 Schalke

Stuttgart 1-3 Frankfurt

M’gladbach 3-0 RB Leipzig

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Mwanamke makanika awa kielelezo kwa wengine Lamu

Njaa yamwongezea Ruto presha ya kazi

T L