Austria wapepeta North Macedonia na kuvuna ushindi wao wa kwanza katika historia ya Euro

Austria wapepeta North Macedonia na kuvuna ushindi wao wa kwanza katika historia ya Euro

Na MASHIRIKA

WACHEZAJI Marko Arnautovic na Michael Gregoritsch walifunga bao kila mmoja na kusaidia Austria kucharaza Macedonia Kaskazini 3-1 katika mechi ya Kundi C kwenye fainali za Euro mnamo Juni 13, 2021.

Ilikuwa mara ya kwanza kwa Austria ya kocha Franco Foda kusajili ushindi kwenye kampeni za kivumbi hicho kilichowakutanisha na limbukeni Macedonia.

Gregoritsch alifunga bao lake katika dakika ya 78 baada ya kukamilisha krosi ya David Alaba. Arnautovic alizamisha kabisa matumaini ya Macedonia kunako dakika ya 89 alipomwacha hoi kipa Stole Dimitrievski. Awali, fowadi Stefan Lainer alikuwa amewaweka Austria kifua mbele katika dakika ya 18 kabla ya juhudi zake kufutwa na mfumaji veterani Goran Pandev katika dakika ya 28.

Macedonia Kaskazini kwa sasa watakutana na Ukraine katika mchuano wao ujao mnamo Juni 17 huku Austria wakivaana na Uholanzi.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Bidco yazidi kupanua biashara zake barani Afrika

Uholanzi wakanyaga Ukraine 3-2 kwenye Euro