Azimio yaonya polisi kuhusu maandamano

Azimio yaonya polisi kuhusu maandamano

WAFUASI

“Askari msije mkatumiwa Jumatatu. Nataka mjue duniani hata Wafaranasa, Israeli na Belarus wanaandamana. Msitumiwe vibaya ilhali maandamano ni haki ya raia ya kikatiba,” akasema Bw Musyoka akiwahutubia wafuasi wa Azimio eneo la Ruaraka.

Seneta wa Narok Ledama Ole Kina pia aliwaeleza polisi kwamba, maadili yao ya kazi haiwaruhusu kukiuka haki za raia na kuwataka wasitumie maandamano ya Jumatatu kuwaua raia hata wakiamrishwa kufanya hivyo.

“Raila amewapigania wananchi kwa miaka mingi na sasa wananchi wameamua kujipigania wenyewe. Kama unajijali, jitokeze Jumatatu kwa sababu serikali hii imeonyesha haiwajali. Polisi wasikubali kutumiwa vibaya kuwaadhibu raia wanaopigania haki,” akasema Seneta huyo.

Akizungumza mjini Nyeri, Bw Gachagua alisema maandamano hayo ya upinzani yanalenga kuharibu biashara zinazomilikiwa hasa na jamii ya Wakikuyu.

Jijini Nairobi, baadhi ya wafanyabiashara walielezea hofu ya kutofungua biashara zao Jumatatu.

Madereva wa magari ya uchukuzi walieleza Taifa Jumapili kwamba, hawatadhubutu kuweka magari yao barabarani licha ya upinzani kusisitiza kuwa maandamano hayo yatakuwa ya amani.

“Hiyo siku sipo kazini kwa sababu siwezi kuhatarisha gari langu. Mimi nafahamu yaliyotokea kwenye maandamano yaliyofanyika miaka ya nyuma,” akasema mmoja wa madereva wa Utimo, magari ambayo husafirisha abiria kutoka Nairobi hadi mtaani Umoja.

Vijana katika mitaa mbalimbali kama Umoja, Kibera na Mathare nao waliahidi kushiriki maandamano hayo huku wakidai serikali imeghairi nia kuhusu ahadi ilizotoa wakati wa kampeni.

Mjini Kisumu, wanasiasa wa ODM waliahidi kuwasafirisha wafuasi wao hadi jijini Nairobi kushiriki maandamano hayo. Wakati wa mkutano wa kisiasa katika uwanja wa Ahindi, Siaya wiki hii, wabunge wa ODM na Gavana James Orengo waliahidi kukodisha mabasi ya kusafirisha wafuasi wao hadi Nairobi.

“Tunakuja Nairobi, baadhi watafika Jumapili asubuhi na wengine jioni. Hata wenzetu kutoka Magharibi wanakuja huko. Sisi kama viongozi tunahusika pia na safari hizo,” Diwani wa wadi ya Milimani, Kisumu Seth Kanga maarufu kama Adui Nyang’ akaeleza Taifa Jumapili.

Na jana Jumamosi, Naibu Rais aliendelea na ziara zake katika ngome zake za kisiasa eneo la Mlima Kenya ambapo alihimiza wenyeji kususia maandamano hayo ya Jumatatu.

Kando na Kenya, maandamano kesho Jumatatu dhidi ya serikali yataendelea Afrika Kusini na Tunisia.

  • Tags

You can share this post!

MALEZI KIDIJITALI: Mipaka idumu hata mtoto akiwa kwa...

‘Maandamano yetu si ya fujo’

T L