Habari Mseto

Azuiliwa kwa kumuua rafikiye aliyemdai Sh500

August 27th, 2020 1 min read

Na Joseph Ndunda

Mkurugenzi wa kuendesha mashtaka wa DCI anazuilia mwendesha  bodaboda aliyeua rafikiye aliyemdai Sh500.

Martin Mungai anayejulikana kama Sparta alimdunga kisu mwendazake kwa kukosa kumlipa deni .

Mshukiwa alikuwa mafichoni hadi Jumamosi iliyopita wakati alikamatwa kwa wizi wa bodaboda.

Bw Mungai aliachilia baada ya kutatua jambo hilo na mmiliki wa  pikipiki lakini  akakamatwa tena baada ya kugunduliwa kwamba alikuwa anatafutwa  kwa kosa la  mauaji.

Koplo Moses Kirima wa DCI Dandora alimuomba  jaji mkuu Derrick Kuto kumruhusu aendelee kumuzuia Bw  Mungai kwa siku 14 lakini lakini mshukiwa huyo alipinga hayo kupitia kwa wakili wake.

Bw Kuto aliruhusu Mungai aendelee kuzuiliwa na ajiwasilishe kortini Septemba 3.