HabariSiasa

'Baba' akutana na Mzee Moi

April 12th, 2018 1 min read

Na WYCLIFFE MUIA

KINARA wa upinzani Raila Odinga Alhamisi amemtembelea Rais mstaafu Daniel arap Moi nyumbani kwake Kabarak, katika Kaunti ya Nakuru.

Bw Odinga alikuwa ameandamana na mbunge wa Mvita Abdulswamwad Shariff Nassir na Seneta wa Vihiga George Khaniri.

Baada ya kuwasili katika uwanja mdogo wa ndege wa Kabarak, Bw Odinga alilakiwa na mbunge wa Tiaty William Kamket na mwenzake wa Moiben Silas Tiren.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga akaribishwa nyumbani kwa rais mstaafu Daniel Moi na mwanawe na pia senata wa Baringo Gideon Moi. Picha/ Hisani

Seneta wa Baringo Gideon Moi pamoja na Katibu Mkuu wa Kanu Nick Salat walimkaribisha Bw Odinga nyumbani kwa rais huyo mstaafu.

“Bw Odinga amemtembelea rais mstaafu Moi ili kumtakia uponyaji wa haraka baada ya kupata matibabu nchini Israeli,” ilisema taarifa kutoka kwa msemaji wa Bw Odinga, Dennis Onyango.

Bw Onyango pia alisema viongozi hao wawili walizungumzia masuala ya kitaifa katika mkutano wao wa zaidi ya saa moja.