Babu Owino aachiliwa kwa dhamana ya Sh10 milioni pesa taslimu

Babu Owino aachiliwa kwa dhamana ya Sh10 milioni pesa taslimu

Na RICHARD MUNGUTI

MBUNGE wa Embakasi Mashariki Paul Ongili maarufu Babu Owino ameachiliwa kwa dhamana ya Sh10 milioni pesa taslimu katika kesi aliyoshtakiwa kwa kumpiga risasi DJ ambapo inalazimika Sh2.5 milioni zilipwe mara moja kabla aruhusiwe kuondoka katika gereza la Viwandani, Nairobi.

Katika uamuzi wa Jumatatu jioni, mahakama imesema pesa zitatumika kugharimia bili ya hospitali ya DJ Evolve ambaye jina lake halisi ni Felix Odhiambo Orinda.

Dhamana hiyo ya pesa taslimu itatolewa kwa awamu nne.

Pia mahakama imeagiza kwamba wabunge wawili wanafaa kutia saini ndipo Babu aachiliwe.

Viongozi hao ni mbunge wa Mathare Anthony Oluoch na seneta maalum Beatrice Kwamboka.

You can share this post!

TAHARIRI: Jamii yafaa ijitolee kuzima ‘usponsa’

‘Tangatanga’ wataka vijana wasio na kazi walipwe

adminleo