Dhamana ya Babu Owino yaangaziwa upya

Dhamana ya Babu Owino yaangaziwa upya

Na JOSEPH WANGUI

JAJI Luka Kimaru ameiangazia upya dhamana ya Mbunge wa Embakasi Mashariki Paul Ongili maarufu kama Babu Owino.

Ametakiwa alipe dhamana ya Sh10 milioni na wadhamini wawili wa kiwango sawa na hicho au alipe Sh5 milioni pesa taslimu katika kesi ya jaribio la kutaka kumuua DJ Evolve kwa risasi katika B Club katika Galana Road, Nairobi mnamo Januari.

Pia ametakiwa awasilishe mahakamani paspoti yake ya usafiri hadi kesi itakapokamilika au pale korti itatoa maagizo mengine kuihusu.

Akitoa uamuzi Jumanne asubuhi jaji amesema viongozi wa mashtaka wa upande wa serikali walishindwa kutoa sababu za kina za mbona masharti ya dhamana hayafai kuangaliwa upya.

Upande wa serikali pia ulitaka dhamana ya mbunge huyo itupiliwe mbali ukisema Babu ana kesi zingine.

Owino aliachiliwa kwa dhamana ya Sh10 milioni pesa taslimu Januari 27, 2020, lakini masharti yakawa awe akilipa kwa awamu nne.

Akitoa uamuzi, Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Milimani Bw Francis Andayi alisema pesa hizo zingetumika kugharimia bili ya matibabu ya Felix Odhiambo Orinda ambaye ndiye DJ Evolve.

Bw Andayi amejiondoa kwa kesi hiyo baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji kuibua pingamizi kwa dhamana hiyo yenye utata.

Mbunge Owino alikamatwa naada ya tukio la ufyatuaji risasi katika B Club jijini Nairobi.

You can share this post!

TAHARIRI: Tuambiwe ukweli wa ziara ya Somalia

SHINA LA UHAI: Sababu za wewe kufanya mazoezi kupunguza...

adminleo