Habari za Kitaifa

BAJETI 2024/25: Pombe kutozwa VAT kwa mujibu wa kiwango cha kileo

June 13th, 2024 1 min read

NA SAMMY WAWERU

USHURU (VAT) wa pombe utakuwa ukitozwa kwa mujibu wa kiwango cha kileo.

Waziri wa Fedha, Prof Njuguna Ndung’u amesema hayo Alhamisi, Juni 13, 2024 wakati akisoma Makadirio ya Bajeti Mwaka wa Fedha 2024/25.

Prof Ndung’u, kwenye makadirio hayo ya matumizi ya fedha serikalini, alisema pendekezo la kutoza pombe ushuru kulingana na kiwango cha kileo halitaathiri biashara.

“Ninapendekeza kila pombe iwe ikitozwa ushuru kwa mujibu wa kiwango chake cha kileo,” Waziri akasema.

Bia, kwa mfano, lita moja imekuwa ikitozwa ushuru wa Sh142.4, divai Sh243.43 kwa kila lita na pombe za makali zenye zaidi ya asilimia 6 ya kileo Sh356.4 kwa lita.

Katika Makadirio ya Bajeti 2023/24, waraibu wa pombe walipata afueni baada ya serikali kuisaza kwenye mapendekezo ya nyongeza ya VAT.