Dondoo

Baki na mistari yako, demu amuambia jombi

January 25th, 2024 1 min read

NA JANET KAVUNGA

LIKONI, MOMBASA

JUHUDI za jombi wa hapa kumrushia mistari ya mapenzi demu waliyejuana kwa miaka mingi ziligonga mwamba, mwanadada alipomwambia alichelewa kufanya hivyo.

Demu alikuwa akimtamani jamaa kwa muda ambao walikuwa marafiki na aliwakataa wanaume wengine akisubiri jombi arushe chambo.

Jamaa alipokosa kufanya hivyo kwa muda wa miaka miwili, demu alimeza ndoano ya kalameni mwingine na wakaanza kupanga harusi.

Mipango ilipokuwa ikiendelea, jamaa alipata ujasiri wa kumrushia demu mistari naye akamwambia alikuwa amechelewa.

“Nilisubiri kwa miaka mitatu maneno kama hayo kutoka kwako hadi nikachoka. Nasikitika umechelewa na nishapata mshikaji, hivyo jilaumu mwenyewe,” demu alimweleza jamaa.