Balozi wa zamani ajiunga na siasa

Balozi wa zamani ajiunga na siasa

Na WINNIE ATIENO

ALIYEKUWA balozi wa Kenya nchini Zambia, Sophie Kombe, amejiunga na siasa.

Bi Kombe anamezea mate kiti cha eneobunge la Kilifi Kusini.

Aliwaomba viongozi wa kidini kumuunga mkono wakati anapojiandaa kuanzisha kampeni zake.Hata hivyo, aliwaonya wanasiasa dhidi ya kuleta vurugu hasa wakati huu wa kampeni.

“Ikiwa kuna vita, ni akina mama na watoto ambao wanaathiriwa zaidi,” akasema.

You can share this post!

Lewandowski afunga mabao mawili na kusaidia Bayern...

Kampuni yafuta shoo ya Olomide jijini

T L