Makala

BAMBIKA: Bae mpya ninaye, ila mimba ndiyo kidogo bado

November 8th, 2019 1 min read

Na THOMAS MATIKO

MTANGAZAJI maarufu wa runinga Betty Kyalo kakanusha tetesi kuwa kanasa ujauzito wa ‘bae’ wake mpya ikiwa ni wiki chache tu baada ya kuanza kumposti mitandaoni.

Toka atemane na mtangazaji wa runinga Dennis Okari, baada ya ndoa ya miezi sita tu, jina la Betty limekuwa likitawala sana Showbiz.

Baadaye alikiri kuwa kwenye uhusiano na Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho ambao haukuenda sawa.

Toka wakati huo Betty aliamua kuwa msiri na maisha yake ya binfasi na mpaka sasa licha ya kuthibitisha kanasa chuma kingine, hajamweka wazi.

Lakini kutokana na mapenzi ambayo amekuwa akionyesha kuyapata huku akionekana kama vile kaongeza unene, wadau wakajijazia kuwa msupa kanasa ball ya pili kitu ambacho kakana.

“Jamani sina ujauzito wowote wala sitarajii mtoto,” Betty kakanusha tetesi hizo.

Betty ana binti kutokana na uhusiano wake na Okari.