Makala

BAMBIKA: Nyimbo zilizozimwa kwa kuonwa 'takataka'

April 19th, 2019 1 min read

Na THOMAS MATIKO

NISHIKE (Sauti Sol)
KUTAZAMWA: 2.9 milioni+

BENDI ya Sauti Sol ilitrendi 2014 baada ya kuachia video ya wimbo huu.

Japo baadhi ya stesheni za TV nchini zilihofu kuucheza kutokana na picha zake za visa vya chumbani, YouTube ilitoa fursa hiyo kwa mashabiki kuitazama tena na tena.

KFCB kupitia Ezekiel Mutua iliishia kupiga marufuku wimbo huo ikiutaja kuwa mchafu na usiostahili kuchezwa kwenye vyombo vya habari.
Hatua hivyo, marufuku iliishia kuisukuma sana video ya Nishike kutokana na mitazamo mseto iliyoibua.

Ni kutokana na hali hiyo wimbo huo uliishia kuteuliwa kwenye tuzo za Channel O Music Video Awards katika kitengo cha Video Bora Afrika Mashariki.

Nishike ilifunga mwaka huo 2014 ikiwa ndio video iliyotazamwa sana Youtube ikivutia zaidi ya views 2.9 milioni.


MELANIN (Sauti Sol
x Patoranking)
KUTAZAMWA: 14.4 milioni+

Miaka miwili iliyopita, Sauti Sol waliachia tena video nzito Melanin wakishirikiana na staa wa Nigeria, Patoranking.

Video iliwahusisha sana vichuna wenye rangi nyeusi wikiwa wamevalia bikini.

Maudhui ya wimbo yalikuwa ni kusifia watu wenye ngozi nyeusi.

Hata hivyo, KFCB iliutaja wimbo huo kuwa mchafu kutizamwa na familia na kuupiga marufuku. Matokeo yake ikawa ni kuipa kiki zaidi na kuvutia utazamaji mkubwa kiasi cha kutizamwa na zaidi ya watu milioni 14. kufikia mwisho wa mwaka huo.