Makala

BAMBIKA: Wako mitini

April 12th, 2019 1 min read

Na THOMAS MATIKO

KULE Bongo kuna msemo “kutesa kwa zamu”.

Wapo wasanii wa kileo waliowahi kutesa sana kwenye chati za muziki duniani kwa miaka mingi katika miaka ya 90 kuelekea 2000 kabla ya kutoweka ghafla bila ya taarifa walikokwenda.

Hawakuelezea sababu na wala hawakuwahi kujaribu kurudi tena kwenye gemu. Waliingia mitini huku nyuma wakiacha nyuma mashabiki wao wakijiuliza kulikoni?

Cha kushangza hata zaidi ni kwamba wasanii hawa, walipotea kwa wakati mmoja utadhania ni kama vile walipanga. Hawa ni Eve, Keyshia Cole, Mary J Blige, Lil Kim, Keri Hilson, na Missy Elliott.

KERI HILSON

Mwaka 2018 mkali huyu wa RnB na Hip Hop miaka ya nyuma alitua Kenya kupiga shoo.

Hii ni licha ya kwamba Hilson hajawahi kuachia muziki kwa zaidi ya miaka saba sasa.

Muziki wake ulikuwa mnene. Alihusika kwenye kolabo na wasanii wakubwa kubwa kama vile Kanye West, Chris Brown miongoni mwa wengine na zote ziliishia kuwa hiti.

Lakini ilifikia wakati akawa kimya na mpaka wa leo hajaachia kazi mpya.

Kwenye mahojiano ya mwaka 2018 Keri alisema sababu ya ukimya wake ilitokana na msongo wa mawazo.