Michezo

Bandari yakamilisha ziara ya Afrika Kusini kwa kuizima Rangers 1-0

June 28th, 2019 1 min read

Na GEOFFREY ANENE

BAO la Yema Mwana lilitosha Bandari FC kuzamisha wenyeji wao Royal Rangers katika mechi ya mwisho ya kujipiga msasa mjini Cape Town nchini Afrika Kusini, Alhamisi.

Mshambuliaji huyu matata, ambaye ni mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, alitikisa nyavu dakika ya 85 na kuhakisisha mabingwa hawa wa Kombe la Ngao (SoportPesa Shield) mwaka 2015 na 2019 Bandari.

Mwana alifungia Bandari mabao 12 kwenye Ligi Kuu ya Kenya msimu uliopita wa 2018-2019 akimaliza nyuma ya Enosh Ochieng’ wa Ulinzi Stars (mabao 18), Allan Wanga wa Kakamega Homeboyz na Mganda Umaru Kasumba wa Sofapaka (17 kila mmoja) na Cliff Nyakeya (Mathare United) na Derrick Otanga (SoNy Sugar) waliotikisa nyavu mara 13 kila mmoja.

Mechi ya kwanza

Katika mechi ya kwanza, Bandari ilitoka 2-2 dhidi ya wenyeji wao Cape Town City.

Bandari ya kocha Bernard Mwalala ilipata mabao kupitia kwa Mganda William Wadri na Benjamin Mosha.

Nayo Cape Town City ya kocha Benni McCarthy iliona lango kupitia kwa Chris David na Siphelele Mthembu.

Bandari sasa inatarajiwa kurejea nyumbani ili kuanza kujiandaa kwa soka ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa Kagame Cup) itakayofanyika Julai 6-21 nchini Rwanda. Imetiwa katika kundi moja na mabingwa watetezi Azam (Tanzania) pamoja na Mukura (Rwanda) na KCCA (Ugand

 

Kocha Bernard Mwalala wa Bandari FC akiwa na Benni McCarthy. Picha/ Hisani