Habari Mseto

Bangi ya Sh400,000 yanaswa Nyali

October 4th, 2020 1 min read

NA MOHAMED AHMED

Polisi katika Kaunti ya Mombasa wamepata misokoto kadhaa ya bangi vya dhamana ya Sh400,000.

Mwanamke anayeaminika kuendesha biashara hiyo alikamatwa kwenye operesheni iliyofanyikakatika eneo la Nyali.

Mshukiwa huyo alikamatwa nyumbani kwake Mkunguni Bombolulu usiku na mmafisa waa polisi kutoka Mombasa.

Kwenye taarifa ya polisi iliyoonekana na Taifa Leo bangi hiyo ilikuwa imefungwa kwa misokoto mitano mitano  na kuwekwa kwa mifuko.

“Mshukiwa huyo alikuwa akisambaza bangi hiyo kupitia gari lenye nambari la usajili KCY681M. Mshukiwa huyo alifikishwa kituo cha polisi cha Kadzandani,” ilisema ripoti hiyo.

Atafikishwa kortini Jumatatu kujibu mashataka ya ulanguzi wa dawa za kulevya.

Kulingana na habari za polisi dereva wa gari hilo aina ya Toyota Ractis alifanikiwa kuhepa.

“Gari hilo ni la kutoka Kaunti ya Migori ambapo kunaaminika kuwa bangi hiyo ilitoka. Dereva huyo alikuwa na bahati kuhepa,” zilisema habari ya polisi.