Bangi yanaswa ikisafirishwa kwa basi la Dreamline

Bangi yanaswa ikisafirishwa kwa basi la Dreamline

NA SAMMY KIMATU

MAAFISA wa upelelezi katika eneo la Makadara wamewakamatwa washukiwa watatu kwa kudaiwa kuwa walanguzi wa mihadarati.

Mkuu wa polisi katika eneo hilo, Bw Makadara Timon Odingo alisema maafisa wa DCIO walikuwa wamepashwa habari na wananchi kuhusu usafirishaji wa dawa za kulevya kupitia kwa basi lililokamatwa.

Basi hilo lilikamatwa likiwa katika barabara ya Mombasa Road karibu na dukakuu la Quickmart jijini Nairobi.

Basi hilo lilikuwa likielekea Mombasa.

Kinara wa DCIO, Bw Felix Kituku Kithuku ameambia Taifa Leo baada ya upekuzi kufanywa, sanduku lililokuwa na dawa hizo lilinaswa.

“Maafisa hao walifanya upekuzi kwenye buti za gari hilo na kupata kijisanduku kimoja chenye misokoto mikubwa mirefu 100 ya bangi yenye thamani ya Sh150,000 bei ya mtaani. Kondakta na madereva wawili wa basi hilo hawakuweza kueleza kuhusu mzigo huo. Abiria wote pia walikataa kuhusishwa na mizigo hiyo,” Bw Kithuku amesema.

Madereva hao wawili ambao ni Bw Khalfan Njoroge Kimani mwenye umri wa miaka 51, Bw Khamis Hassan Awadh, 38 na kondakta Bw Christopher Kivuva wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Industrial Area.

“Sasa hivi, washukiwa watatu wamezuiliwa katika kituo cha Polisi cha Industrial Area ili wahojiwe na maafisa wangu kabla ya kufunguliwa mashtaka,” Bw Kithuku akasema.

Ameongeza kuwa basi hilo lilivutwa hadi kituoni humo baada ya abiria waliokuwemo kupatiwa gari tofauti na kuendelea na safari.

Basi hilo la Dreamline Express ni la muundo wa Scania na lina nambari za usajili KCK 266C.

  • Tags

You can share this post!

WANTO WARUI: Serikali iweke mipango madhubuti ya masomo ya...

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Croatia kwenye mizani ya wauaji...

T L