Habari Mseto

Barakoa zisiuzwe zaidi ya Sh20 – Serikali

April 3rd, 2020 1 min read

Na CHARLES WASONGA

WAZIRI wa Biashara na Viwanda Betty Maina ametangaza kuwa barokoa ambazo zitatolewa na serikali kwa umma zitauzwa kwa kati ya Sh5 na Sh20.

Akiongea na wanahabari jana, Nairobi , Bi Maina alisema wizara tayari imetambua kampuni za humu nchini ambazo zitatengeneza vifaa hivyo kwa wingi ili visambazwe kote nchini.

“Nina uhakikisha kuwa kampuni za humu nchini zitatengeneza vifaa hivyo kwa wingi na hivyo tutawez kuwasambazia wananchi kwa bei nafuu ya Sh5 na Sh20 ikiwa juu zaidi.

Mnamo Alhamisi Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alitangaza kuwa sasa wahudumu wa matatu, pikipiki na Tuk tuk pamoja na abiria wao watahitajika kuvalia barokoa kwenye nyuso zao.

Alisema hii sehemu ya hatua za watu kujikinga kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Kampuni ya kutengeneza nguo ya Rivatex ni miongoni mwa kampuni za humu nchini ambazo zimetangaza kuwa zitatengeneza vifaa hivyo kwa wingi.

Jana, wachuuzi walikuwa wakiuza vifaa hivyo kwa kati ay Sh100 na Sh50 katikati mwa jiji la Nairobi.

Hata hivyo, Bi Maina aliwaonya wananchi dhidi ya kununua barokoa feki zilizotengeneza kwa malighafi feki akisema haziweze kuzuia virusi vya corona.