Barbara Waweru ‘Mama Nyambu’ ni mwigizaji anayepania kutinga hadhi ya kimataifa

Barbara Waweru ‘Mama Nyambu’ ni mwigizaji anayepania kutinga hadhi ya kimataifa

NA JOHN KIMWERE

PENYE nia pana njia.

Ndivyo wahenga walivyolonga na tangia zama zile ndivyo hali ilivyo hadi sasa.

Ni msemo unaonekana kuwa na mashiko kwa kiwango fulani katika jamii yoyote.

Pia ni msemo huu unaendelea kuthibitishwa na vijana wengi wavulana kwa wasichana wanaojitosa kuchangamkia shughuli tofauti kwenye jitihada za kusaka riziki.

Barbara Nyambura Waweru maarufu Mama Nyambu ni kati ya waigizaji wa kike wanaoibukia wanaopania kutinga hadhi ya kimataifa miaka ijayo. Kando na uigizaji dada huyu ni meneja wa shirika la kidijitali la Universal Music Kenya.

”Bila kujipigia debe ninahisi nina talanta ya uigizaji ambapo nina ndoto ya kuibuka msanii mahiri nchini na duniani miaka ijayo kwa mapenzi yake Muumba,” anasema na kuongeza kuwa anafahamu mtaka cha mvunguni sharti ainame jambo analolifanyia kazi.

Msichana huyu alianza kujituma kwenye masuala ya uigizaji mwaka 2014 alipojiunga na kundi la Strathmore Drama Society. Mengine yakiwa FCA, Hearts of Art, Tini Tiny Tone na Mamlaka Chapel.

Anadokeza mapenzi yake katika maigizo ndiyo yalimchochea kuanza kujiunga na tasnia hii.

Anaponda serikali kwa kutofadhili sekta ya uigizaji wala kuweka mikakati ya ubunaji wa sheria za kusaidia tansia hii kupiga hatua na kutoa nafasi za ajira kwa wahusika.

Katika mpango mzima amepania kufuata nyayo za waigizaji mahiri duniani kama Viola Davis mzawa wa Marekani aliyeshiriki filamu kama ‘Fences’ na ‘The help’ kati ya nyingine.

Anasema kuwa tangia akiwa mtoto alitamani kuhitimu kuwa rubani ila mambo hayakuenda alivyotarajia.

”Licha ya kwamba sijapiga hatua kubwa kwenye masuala ya uigizaji nitafurahi sana endapo nitafanikiwa kumiliki brandi yangu miaka ijayo,” akasema.

Afrika angependa kufanya kazi nao Charlize Theron pia Thandie Newton wazawa wa Afrika Kusini na Zimbabwe ambao hushiriki filamu za Hollywood.

Wawili hao wameshiriki filamu kama ‘Fast and Furious’,¬†Atomic Blonde’ na ‘All the old knives’ pia ‘Crash’ mtawalia.

Hapa nchini itakuwa furaha kwake endapo atajipata jukwaa moja na wanamaigizo kama Mkamzee Mwatela na Lupita Nyong’o ambaye hushiriki filamu za Hollywood.

Mkamzee ameshiriki filamu kama ‘Mali’ na ‘Lusala’.

Naye Lupita alitamba na filamu kama ‘Black Panther’ na ’12 Years A Slave’.

Anasema kuwa ingawa anachukulia uigizaji kama ajira kwa muda bado hajafaulu kupata matunda yake vizuri.

Kamwe binti huyu si mchoyo wa mawaidha.

Anashauri wenzie wawe na subira, wajiamini kwa kile wanachofanya wala wasivunjike moyo.

”Sina shaka kutaja kuwa wengi tuna kipaji cha uigizaji lakini hushindwa kujitambua na kujihusisha na masuala ambayo baadaye hutuharibia taaluma yetu,” anasema.

  • Tags

You can share this post!

Ulinzi Starlets pazuri kumaliza katika nafasi ya pili KWPL

Makipa Ederson na Alisson wa Man-City na Liverpool mtawalia...

T L