Barcelona wacharaza Real Sociedad 1-0 na kuingia nusu-fainali za Copa del Rey

Barcelona wacharaza Real Sociedad 1-0 na kuingia nusu-fainali za Copa del Rey

Na MASHIRIKA

OUSMANE Dembele alifunga bao la pekee na la ushindi dhidi ya Real Sociedad na kusaidia Barcelona kutinga nusu-fainali ya Copa del Rey msimu huu wa 2022-23.

Wageni Sociedad walioshuka dimbani wakijivunia rekodi ya kushinda mechi tisa mfululizo, walikabiliwa na pigo baada ya mchezaji wao Brais Mendez kuonyeshwa kadi nyekundu kwa hatia ya kumchezea Sergio Busquets visivyo katika kipindi cha kwanza.

Bao la Dembele katika dakika ya 52 lilikuwa zao la ushirikiano mkubwa kati yake na Jules Kounde. Gavi nusura afungie Barcelona bao la pili katika kipindi cha pili ila kombora lake likagonga mwamba wa goli la Sociedad.

Osasuna nao walijikatia tiketi ya kunogesha nusu-fainali za Copa del Rey msimu huu baada ya kutandika Sevilla 2-1 katika muda wa ziada.

Ezequiel Avila alidhani alikuwa ameshindia Osasuna mechi hiyo katika muda wa kawaida ila Sevilla wakasawazisha kupitia kwa Youssef En-Nesyri kunako dakika ya 94. Fowadi Abde Ezzalzouli anayechezea Osasuna kwa mkopo kutoka Barcelona, alipachika wavuni bao la ushindi.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Afisa wa polisi aagizwa ajisalimishe bila kupoteza hata...

Man-United guu moja ndani ya fainali ya Carabao Cup baada...

T L