Barcelona wakomoa Sevilla na kufungua mwanya wa alama nane kileleni mwa jedwali la La Liga

Barcelona wakomoa Sevilla na kufungua mwanya wa alama nane kileleni mwa jedwali la La Liga

Na MASHIRIKA

BARCELONA walifungua mwanya wa alama nane kati yao na nambari mbili Real Madrid kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) baada ya kukomoa Sevilla 3-0 mnamo Jumapili ugani Camp Nou.

Wenyeji Barcelona waliwekwa kifua mbele na Jordi Alba katika dakika ya 58 kabla ya Pablo Gavi na Raphinha Belloli kupachika magoli mengine wavuni kunako dakika za 71 na 79.

Huku Barcelona wakiselelea kileleni mwa jedwali kwa alama 53, matokeo hayo yalisaza Sevilla katika nafasi ya 16 kwa pointi 21 sawa na Espanyol.

Hata hivyo, raha ya ushindi huo wa Barcelona iliyeyushwa na jeraha la kifundo cha mguu lililomlazimisha nahodha Sergio Busquets kuondolewa uwanjani baada ya dakika nne pekee za kipindi cha kwanza.

Barcelona watakuwa wenyeji wa Manchester United katika mkondo wa kwanza wa hatua ya 16-bora ya Europa League mnamo Februari 16 ugani Camp Nou.

Mapema Jumapili, mabingwa watetezi wa La Liga, Real Madrid walipoteza fursa ya kukaribia Barcelona kileleni mwa jedwali baada ya kuduwazwa na Mallorca kwa kichapo cha 1-0 ugenini.

MATOKEO YA LA LIGA (Jumapili):

Mallorca 1-0 Real Madrid

Barcelona 3-0 Sevilla

Girona 1-0 Valencia

Sociedad 0-1 Valladolid

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Chepng’etich arejea mbio za nyika kwa kishindo,...

Wafugaji wapinga New-KCC kubinafsishwa

T L