Barcelona wamtia Messi kwenye orodha ya masogora watakaowachezea muhula ujao wa 2021-22

Barcelona wamtia Messi kwenye orodha ya masogora watakaowachezea muhula ujao wa 2021-22

Na MASHIRIKA

LIONEL Messi atasalia kuwa mchezaji wa Barcelona baada ya kikosi hicho kumtia katika orodha ya wachezaji ambao wamesajiliwa kukiwajibikia kwenye kampeni za muhula ujao wa 2021-22.

Orodha hiyo tayari imeidhinishwa na vinara wa Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) ambao kulingana na gazeti la Mundo Deportivo, wamethibitisha kuwa gharama ya kudumishwa kwa Messi ugani Camp Nou hakutakiuka kanuni za matumizi ya fedha kwa mujibu wa Shirikisho la Soka barani Ulaya (Uefa).

Inaarifiwa kwamba rais wa Barcelona Joan Laporta na Jorge ambaye ni baba na wakala wa Messi, wameafikiana kuhusu mkataba mpya wa miaka miwili ambao sogora huyo raia wa Argentina atatia wino wakati wowote kuanzia sasa.

Vikosi vingine ambavyo vimekuwa vikiwania huduma za Messi ni Manchester City na Paris Saint-Germain (PSG) vya Uingereza na Ufaransa mtawalia.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Nairobi, kaunti za Mlima Kenya zaorodheshwa tajiri zaidi...

Lengo la Uingereza kwa sasa ni kutwaa Kombe la Dunia 2022...